Kilabu ya Azam kutoka Tanzania imefuzu katika fainali ya ombe la Kagame
CeCAFA baada ya kuindoa KCCA ya Uganda kwa bao moja kwa bila katika
mechi ya nusu fainali ya pili iliochezwa katika uwanja wa kitaifa wa
Dar-es-Salaam nchini Tanzania.
Hatua hiyo inaaminisha kwamba Kilabu ya Gor Mahia ya Kenya itakabiliana na Azam katika fainali ya Kombe la CECAFA.Azam ilihitaji bao la dakika za mwisho lililofungwa na Farid Musa kuilaza KCCA kutoka Uganda na kufuzu katika awamu ya kilele cha kombe hilo.
Post a Comment